Hatimaye uchaguzi mdogo wa Jimbo la Liwale umemalizika huku mgombea wa chama cha mapinduzi (CCM), Zuberi Kuchauka akiibuka mshindi wa kiti cha ubunge.
Msimamizi wa uchaguzi Jimboni hapo, Luiza Mlelwa amesema kuwa waliojiandikisha kupiga kura walikuwa 55777 na waliojitokeza kupiga kura walikuwa 40706 kura halali zilikuwa 40,301 kura zilizokataliwa ni 405
Akimtangaza mshindi wa kiti cha ubunge wa Jimbo la Liwale msimamizi wa uchaguzi amesema kuwa, Zuberi ameshinda kwa kura 34, 582 sawa na asilimia 85.81
Aidha, mara baada ya kutangazwa mshindi wa kiti cha Ubunge, Zuberi Kuchauka amesema kuwa ameyapokea matokeo hayo kwa furaha na ameahidi kushirikiana na wananchi wa Jimbo la Liwale kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.
Kuchauka amesema kuwa changamoto nyingi zilizopo katika Jimbo la Liwale ni pamoja na miundombinu ya Barabara, Maji, Elimu, Mawasiliano na Afya ambapo ameahidi wananchi kuwa atashughulikia changamoto hizo.
Kwa upande wake, Abdul Kombo Ngakolwa ambaye ni mgombea wa Chama cha (AAFP) chama cha wakulima amesema ameridhishwa na ushindi alioupata mgombea wa (CCM) na amempongeza kwa ushindi huo.
“Mara zote mtu unaposhindana lazima mmoja ashinde, asiyekubali kushindwa siyo mshindani” amesema Kombo
-
Breaking News: Mbunge Mwingine Chadema ajiuzulu na kuomba kuhamia CCM
-
Mbunge mwingine wa Chadema ajiuzulu
-
Mbowe ajibu mapigo, adai Chadema ilishiriki msiba wa ajali ya MV. Nyerere
Hata hivyo, mchakato wa kumtafuta mbunge wa Jimbo la Liwale ulianza mwezi mmoja uliopita ambapo waliotangaza nia ya kuwania kiti hicho ni wagombea kutoka vyama vya AAFP kura 18 sawa 0.2% (UMD 109 sawa 0.49% ACT- Wazalendo 285 sawa na 0.79%, CUF 5207 sawa na 12. 92%.