Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimetoa siku 14 kwa Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Angellah Kairuki kufika kituo cha afya Mikese, Morogoro ili kujua chanzo cha kutelekezwa kwa majengo ya huduma ya mama na mtoto kwa zaidi ya miaka mitatu.

CCM imeyasema hayo kupitia kwa Katibu Mkuu wake Taifa, Daniel Chongolo baada ya kuwasili katika kituo hicho cha afya ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku tisa mkoani humo.

Amesema, haiwezekani kuona serikali imewekeza zaidi ya shilingi milioni 400 katika ujenzi wa miundombinu hiyo ya afya, lakini bado hakuna tija kwa wananchi na majengo hayo kukaa bila kufanya kazi iliyokusudiwa.

Kukamilika kwa kituo hicho cha afya Mikese, kulilenga kuwapunguzia adha akina mama wajawazito, kwa kutembea umbali mrefu kufuata huduma za mama na mtoto maeneo ya mbali na hivyo kuwa hatarini na mambo mbalimbali ikiwemo kupoteza muda mwingi safarini.

Mesut Ozil aomba POO Istanbul Basaksehir
Bruno Gomes: Sijui kuhusu Young Africans