Kiungo kutoka nchini Ujerumani Mesut Özil ameutaka Uongozi wa Klabu ya Istanbul Basaksehir kusitisha mkataba wake, baada ya kufikia Uamuzi wa kuachana na soka.

Ozil alisajiliwa na klabu hiyo kwa klabu ya mwaka mmoja mwanzoni mwa msimu huu akitokea Fenerbahçe, na Uongozi wa Istanbul Basaksehir uliamini uwepo wake utaongeza chachu kwa wachezaji wa klabu hiyo.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 34, hakuripoti kwenye mazoezi ya klabu hiyo na tayari ameripotiwa kuwajulisha wachezaji wenzake juu ya Uamuzi huo.

Ozil alikuwa mmoja wa viungo bora kuwahi kutokea katika soka na aling’ara akiwa na Klabu ya Real Madrid ya Hispania na Arsenal ya England.

Hadi sasa Ozil ameshaitumikia Istanbul Basaksehir katika michezo minne ya Ligi Kuu ya Uturuki hadi sasa.

Vifo watu 17: Rais Samia atuma salamu za rambirambi
CCM yampa siku 14 Waziri Kairuki