Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kwa wafiwa kufuatia vifo vya watu 17 waliofariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Magila Gereza, Wilayani Korogwe mkoani Tanga.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Rais Samia ameandika kuwa, “nimesikitishwa na vifo vya watu 17 vilivyosababishwa na ajali iliyotokea jana saa 04:30 usiku eneo la Magila Gereza Wilaya ya Korogwe Mkoa wa Tanga.”

Katika ajali hiyuo, watu 17 wlifariki na wengine 12 kujeruhiwa baada ya Basi dogo walilokuwa wakisafiria kugongana na Lori uso kwa uso usiku wa kuamkia Februari 4, 2023 ikihusisha Lori aina ya Mitsubishi Fuso na Basi dogo aina ya Coaster.

Basi hilo dogo, lilikuwa lilibeba mwili wa marehemu na abiria 26 na lilikuwa likitokea Mkoani Dar es Salaam kwenda Moshi huku chanjo cha ajali hiyo kikiwa ni mwendo kasi na uzembe wa dereva wa fuso aliyekuwa akilipita gari la mbele yake bila ya kuchukua tahadhari.

Neymar kuondoka Paris Saint-Germain
Mesut Ozil aomba POO Istanbul Basaksehir