Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema hakitotoa maelezo juu ya malalamiko yaliyopelekwa kwa msajili wa vyama vya siasa na wabunge wa viti maalum 19 kuhusu kufukuzwa uwanachama baadala yake maelezo yote yatapelekwa kwenye mkutano wa Baraza Kuu wa chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 14,2021 Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Bara, Benson Kigaila amesema mnamo tarehe 6/07/2021 walipokea barua kutoka kwa msajili wa vyama vya siasa yakuwataka kuwasilisha maelezo juu yamalalamiko yalipopelekwa ya kutokukubaliana na tamko la chama la kuwafukuza wanachama.

Aidha Kigaila amesema hawawezi kutoa maelezo kwa Jaji Mutungi kwakuwa ni kinyume cha utaratibu wa chama hicho.

“Sasa msajili akisema hakubaliani na maelezo yetu na kwamba hawa watu 19 ni wanachama halali, si amevuruga  mchakato wa Baraza Kuu?”

Wabunge hao 19, wakiongozwa na Halima Mdee aliyekuwa mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la CHADEMA ( BAWACHA), walifukuzwa uanachama mwaka jana na kamati kuu ya Chadema  baada ya kwenda kinyume na msimamo wa chama hicho kwa hatua yao ya kuapa kuwa wabunge wa viti maalumu bila ridhaa ya chama.

Askari JWTZ akamatwa kwa tuhuma za mauaji
Mgodi wa Tancoal kupewa siku 14 kuthibiti maji taka