Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Hamad Hassan Chande (Kushoto) akipata maelezo uchimbaji wa makaa ya mawe na hifadhi ya mazingira kutoka kwa Edward Mwanga Meneja wa Mgodi wa TanCoal ulipo Mbinga. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Aziza Mangosongo

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Hamad Hassan Chande, ametoa siku 14 kwa Mgodi wa Tancoal kudhibiti maji taka katika mabwawa yao pamoja na kudhibiti vumbi ambalo limeku wa kero kwa wakazi wa maeneo ya jirani.

Ameyasema hayo leo Julai 14, 2021 mara baada ya kufanya ziara ya kukagua migodi ya uchimbaji wa Makaa ya mawe ya Tancoal Ltd na Ruvuma coal.

Amesema kuwa, Serikali inasisistiza uwekezaji wowote ni lazima uzingatie Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 na Kanuni zake ikiwa ni pamoja na kufanya Tathmini ya Athari kwa Mazingira kwa kuwa ni takwa la Kisheria.

Hata hivyo, Naibu Waziri Chande ameagiza migodi hiyo ya makaa ya mawe kuhakikisha wanaanda na kutekeleza mpango madhubuti wa kurejesha ardhi katika hali ya awali mara baada ya shughuli za uchimbaji kukamilika ikiwa ni pamoja na kupanda miti kwa wingi.

“Upandaji miti uwe ni utamaduni wetu, hapa mgodini miti mingi imekatwa, wekeni mkakati wa kuirejesha kipindi cha mvua,” Amesema Naibu Waziri Chande.

Katika hatua nyingine Waziri Chande amemuagiza Meneja wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira Kanda ya Kusini Bw. Jamal Baruti kufanya kaguzi za mara kwa mara ili kuhakikisha masuala ya Uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira yanakuwa endelevu.

CHADEMA wamgomea Msajili wa vyama
Vifo vya fikia 72 Afrika Kusini