Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Zanzibar), Salum Mwalimu amesema kwamba matukio yanayoendelea kutokea hayawezi kuwaziba midomo au kusimamisha kazi zao bali yanazidi kuwaimarisha zaidi kisiasa.
Ameyasema jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa chama hicho hakijafungwa mdomo tangu tukio la kupigwa risasi kwa mwanasheria wa chama hicho, Tundu Lissu.
Amesema kuwa tukio la kushambuliwa kwa kiongozi wao hakujafanya chama hicho kushindwa kuendelea na shughuli za chama na badala yake wanaendelea kuimarisha chama.
“Tupo kwenye vikao vizito vya kuhakikisha tunafanya vizuri kwenye uchaguzi mdogo uliotangazwa. tukio hili la Lissu halijafanya shughuli za chama zisimame, Shughuli zinaendelea kama kawaida. Mikoani na makao makuu ya chama mambo yetu yanaenda kama awali,”zmesemz Salum Mwalimu
-
Msigwa: Tuko tayari kuuza kila kitu chetu kugharamia matibabu ya Lissu
-
Diwani amtaka Mbowe kumtafuta Dkt. Slaa
Hata hivyo, kuhusu maendeleo ya Mbunge wa Singida Mashariki, amesema kuwa watatoa taarifa siku chache zijazo, hivyo amewataka wanachama wa chama hicho kuwa watulivu.