Fomu ya rufaa ya Mgombea Ubunge Jimbo la Korogwe Vijijini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Amina Ally Saguti imepokelewa na Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Korogwe, Frolian Kimaro baada ya malumbano ya muda mrefu.
Katika rufaa hiyo Mgombea, Saguti anapinga uamuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Korogwe Vijijini kumtangaza mgombea ubunge wa CCM kuwa amepita bila kupingwa.
Aidha, mgombea huyo akiambatana na Viongozi wa chama hicho Wilaya ya Korogwe, walifika ofisi ya msimamizi kuwasilisha fomu hizo lakini alikumbana na vikwazo.
Fomu na. 12 ilipatikana kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi baada ya Uongozi wa CHADEMA ngazi ya taifa kulazimika kufanya mawasiliano ili kupata fomu hiyo kutokana na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Korogwe kukataa kutoa.
-
Video: Mgombea Ubunge Chadema Jimbo la Korogwe afunguka
-
Video: Tunamtambua Prof. Lipumba, Maalim Seif amesimamishwa- Mwinyi
- Ngome ya Mbowe yazidi kumong’onyoka
Hata hivyo, chama hicho tayari kimeshamwandikia rasmi Mkurugenzi wa NEC kumtaka achukue hatua za haraka kuingilia kati mwenendo wa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Korogwe hasa kubatilisha uamuzi wake uliokiuka taratibu zinazosimamia uchaguzi.