Baadhi ya Watoto nchini, wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali katika maisha wanazozijua ambazo wakati mwingine Wazazi wamekuwa hawazifahamu na hivyo kushindwa kuchukua hatua za utoaji msaada na kukabili nyakati ngumu wanazopitia.

Hayo yamebainishwa na Diwani wa Kata ya Tandale, Abdallah Aziz mara baada ya kumalizikwa kwa Mdahalo ulioandaliwa na Shirika la Save the Children, kwa kushirikiana na Manispaa ya Kinondoni kuhusu uelewa wa mtoto katika jamii inayomzunguka.

Diwani wa Kata ya Tandale, Abdallah Aziz.

Amesema, “dahalo hu umetusaidia kutambua mambo mengi na niseme watoto wamekuwa na changamoto nyingi sana ambazo wao wanazijua na hata wazazi wanaweza kuwa hawazijui kwahiyo tujenge mazoea ya kuwasikiliza itasaidia kuwaondolea mazonge mengi.”

Awali, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa kwa Tumbo iliyopo kata ya Tandale, Hatibu Kibwana alisema watoto kukosa kushiriki katika midahalo kama hiyo wamekuwa wakikosa sehemu ya kusemea moja kwamoja changamoto zao na mawazo yao kwa mambo wanayokabiliana nayo.

Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Manispa ya Kinondoni, Zabrina Salum.

“Sio kila wakati watu wazima ndio wanakuwa na mawazo hata watoto nao wanakuwa wakikumbana na changamoto za kiafya, ukatili na hata kifedha kwahiyo wanapopewa nafasi katika sehemu kama hizi inakuwa ni rahisi sisi wazazi kujua tunaanzia wapi katika utatuzi.

Kwa upande wake Mwenyekiti Manispa ya Kinondoni Baraza la Watoto, Zabrina Salum amesema mbali na mambo mengine ikiwemo ukatili, pia watoto wanatakiwa kushirikishwa ili waseme mambo yanayowakabili hasa katika masuala ya afya kwa minajili ya kuokoa maisha yao.

Robertinho asisitiza umoja Simba SC
Hanscana atoa somo zito kwa wasanii TZ