Charles III mwenye (74), sasa ni mfalme wa Uingereza akichukua nafasi ya mama yake malkia Elizabeth II aliyefariki mwaka jana, halfa ambayo imefanyika kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1953.
Hafla hiyo ambayo imefanyika katika kanisa la Anglikan la Westminster Abbey, imehudhuria na watu maarufu nje na ndani ya Uingereza ikiongozwa na askofu mkuu wa CanterburyJustin Welby.
Mbali na waliohudhuria, pia Mamilioni ya watu duniani walifuatilia sherehe hizo kwa njia ya mitandao, wakishuhudia matukio mbalimbali yaliyojumuisha tamaduni, dini na matamasha.
Sherehe rasmi ziliaanza kwa msafara kutoka Buckingham Palace hadi Westminster Abbey huku maeneo ya kutazama tukio hilo yakiwa kwenye njia iliyofunguliwa saa kumi na mbili asubuhi kwa saa za Uingereza.
Miongoni mwa walioalikwa walikuwa ni washirika wa familia ya Kifalme, waziri mkuu, wawakilishi kutoka mabunge, wakuu wa nchi, na washiriki wengine wa familia ya kifalme kutoka kote ulimwenguni.