Meneja mpya wa Klabu ya Chelsea Mauricio Pochettino ni kama Pochettino amejiingiza kwenye mtego baada ya bosi wa klabu hiyo, Toddy Boehly kusema hatakuwa na muda wa kuvumilia madudu tena.
Ikiwa na maana ku anatakiwa kufanya mabadiliko haraka kwenye klabu ambayo yatakuwa na tija chanya kwenye timu hiyo yenye nyota kibao. Muargentina huyo, 51, anaanza jukumu lake jipya Julai Mosi, 2023
Pochettino ambaye aliwahi kuvinoa vikosi vya klabu za Tottenham na Paris St-Germain alitangazwa kuwa Meneja wa The lues mwishoni mwa juma lililopita akisaini Mkataba wa miaka miwili, ukiwa na kipengele cha kuongezewa mwaka zaidi.
Aliyekuwa Meneja wa muda wa Chelsea Frank Lampard aliipeleka klabu hiyo hadi nafasi ya 12 kwenye Premier League na kumaliza wakiwa chini kabisa kwa zaidi ya miaka 25.
“Mauricio ni kocha wa kiwango cha kimataifa mwenye rekodi bora. Sote tunatazamia kuwa naye kwenye bodi,” klabu hiyo ilisema.
“Wamiliki wa Chelsea hawawezi kuvumilia Pochettino kufanya vibaya. Atahitajika kufanya kazi ya ziada na nzuri kwa muda mfupi.”