Serikali ya nchi ya China, imeifutia Tanzania deni la shilingi billion 31.4 ambalo ilikuwa inaidai Tanzania na kusaini baadhi ya mikataba ya makubaliano, baina ya nchi hizo mbili.
Makubaliano hayo, ni uwepo wa soko la kusafirisha maparachichi toka nchini kwenda China, soko la mabondo ya samaki na vitu vingine vitokanavyo na samaki ambapo pia imeikopesha Tanzania Dola milioni 56.7 kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja wa ndege Zanzibar, terminal III.