Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi – CCM, Daniel Chongolo amemuagiza Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kuhakikisha ndani ya wiki tatu anafika katika kata ya Masaka iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, akiwa ameambatana na timu ya Wataalamu kutoka Wizarani kwake kwa ajili ya kuangalia namna ya kujenga skimu ya umwagiliaji itakayokuwa na tija kwa Wakulima wa eneo hilo.

Chongolo ametoa agizo hilo, baada ya kuzindua upandaji wa samaki katika mradi wa Bwawa la Masaka, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku 7 Mkoani Iringa.

Maelekezo hayo ya Chongolo kwa Bashe, yanakuja kufuatia Malalamiko ya Diwani wa Kata ya Masaka Mathew Nganyagwa kudai tume ya taifa imeshindwa kufika kwenye kata hiyo ili kuweka mifereji ya maji kwenye mabwawa kwa ajili ya kuimarisha shughuli za Kilimo katika Ukanda huo.

“Mimi wala sipigi kelele kwa Sababu umeshasema, najua wale mabwana wanajua wajibu wao, ninakwenda kuzungumza na Waziri wao wa Kilimo ili watafute pesa ya Kujenga Skimu ya Umwagiliaji katika eneo la Upande wa pili kwa Sababu tayari maji yapo,” amesema.

Bwawa la Kisaka, lina ukubwa wa kilomita za mraba 5.33, huku likitarajia kunufaisha Wananchi zaidi ya Elfu Kumi wanaopatikana ndani na nje ya Kata ya Masaka iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.

Tanzania Prisons: Tunaisubiri KMC FC Mbeya
Uongozi Young Africans kukomaa na Mayele