Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo amewataka Watanzania wasikubali kupotoshwa kuhusu Mkataba wa Bandari kwani mkataba huo ni wa CCM na si wa mtu mmoja, akisisitiza kuwa suala hilo lipo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2020 Ibara ya 59 ukurasa wa 92 kuhusu uboreshaji wa Bandari.

Chongolo ameyasema hayo wakati akihutibia wananchi wa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Ruanda Nzovwe, Jijini Mbeya.

Amesema kuna watu wametengeneza uongo ili kusapoti dhamira ya kupotosha uboreshaji wa bandari nchini.

Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo

“Serikali imepewa msukumo na chama kinasimamia kuhakikisha utekelezaji unafanyika, naagiza Serikali ichakate haraka kuelekea kwenye mkataba wa uwekezaji wa Bandari,” amesema Chongolo

“Kazi ya maneno ya siasa ni ya wanasiasa, watendaji wasihangaike kujibu. Eti Jambo la flani hata angekuwa nani ndani ya CCM agenda isiyo na maslahi ya watu haitapita, ilani hiyo ya CCM ndiyo iliyoweka ahadi ya kuboresha bandari zote nchini”.

“Aliyeandaa ilani ndiye aliyeweka haya malengo, mjadala wa Ilani ulianza mwaka 2020. Tuliahidi, baada kuahidi tunatekeleza. Tukicheka na wanaopotosha adhabu itakuwa kwetu,” amesema Chongolo.

Kulingana na Chongolo, takwimu zinaonyesha kuwa bandari kwa sasa inaingiza zaidi ya Sh7 trilioni huku asilimia 99 ya fedha hizo ikitumika kwa matumizi yao wenyewe.

“Nani anakula hizo trilionii Saba? sasa wakiambiwa ulaji unakatwa watafunga midomo? kuna genge la watu wanamlo na hawataki kuona mambo yanabadilika, CCM tuna akili timamu na habari yao wataipata tija ikipatikana. Msikubali, msiyumbishwe agenda ni ya CCM sio ya mtu.” amesema Chongolo.

Chongolo amesema hawezi kusimama na kutetea jambo ambalo haoni tija kwa Watanzania na kuongeza kuwa ikiwa kuna mwana CCM hajasimama kupigania suala hilo lazima kunamashaka na uana CCM wake na sio vinginevyo.

Ruto amshushia lawama Kenyatta
Watoto 289 wafariki wakijaribu kuvuka maji