Ripoti ya Shirika la Uangalizi lisilo la Kiserikali la Global Witness, limeitaja Nchi ya Colombia kuwa ni ya hatari zaidi Duniani kutokana na kuongoza kwa mauaji ya Wanaharakati wa mazingira.
Katika ripoti yake ya kila mwaka, Shirika hilo limesema mauaji dhidi ya wanaharakati wa Mazingira yameongezeka maradufu nchini humo kwa mwaka 2022 huku ikitoa orodha ya watetezi 177 wa ardhi na Mazingira ambao waliuawa mwaka huo huko Ufilipino na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo – DRC.
Aidha, idadi ya waliouawa imepungua ikilinganishwa na rekodi ya watu 227 waliouawa mwaka 2020, lakini Global Witness imesema hali hiyo haimaanishi kuwa kwa kiasi kikubwa hali na unafuu.
Hata hivyo, Shirika hilo pia limesisitiza kuwa kuongezeka kwa mahitaji ya bidhaa za Kilimo, Mafuta na Madini kutazidisha shinikizo kwa Mazingira pamoja na Wanaharakati wanaohatarisha maisha yao, ili kuilinda Mazingira.