Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson kwa mara ya kwanza ametangaza kulegeza vikwazo dhidi ya virusi vya corona.
Johnson amesema kuanzia leo, watu ambao walikuwa hawawezi kufanya kazi wakiwa nyumbani, wanaweza kurudi kazini na wale wanaotaka kufanya mazoezi nje wafanye.
Pia amesema kuanzia Jumatano watu walio na jamaa zao majumbani wanaweza kutoka nje kwa kuzingatia kanuni za umbali wa mtu mmoja na mwengine.
Amesema kuanzia mwezi wa sita mwanzoni, serikali yake itatoa tangazo la iwapo maduka yataanza kufunguliwa taratibu na iwapo wanafunzi wa shule za msingi wataweza kurudi shule.