Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limebadilisha utaratibu wa kuwapokea wageni mbambali kusikiliza vikao vyake.
Taarifa iliyotolewa jana, Machi 19, 2020 na kitengo cha mawasiliano cha Bunge, imeeleza kuwa Spika Ndugai amechukua uamuzi huo kama sehemu ya tahadhari dhidi ya kusambaa kwa virusi vya corona.
Imeeleza kuwa wageni ambao wataruhusiwa kuingia ndani ya bunge hilo ni wale wenye kazi maalum na wenye vibali maalum pekee.
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetangaza kuwa hadi sasa Tanzania ina wagonjwa sita wa virusi vya corona. Kati ya wagonjwa hao, wamo Watanzania ikiwa ni pamoja na watu maarufu. Mwanamuziki Hamisi Mwinjuma (Mwana FA), na meneja wa Diamond Platinumz, Sallam SK ni miongoni mwa waliobainika kuwa na virusi vya corona.
Visa vya corona zaidi ya 220,000 vimebainika duniani kote huku kukiwa na zaidi ya vifo 9,000.