Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale, Mahmoud Thabit Kombo amesema licha ya Zanzibar kutegemea sekta ya Utalii katika uchumi wake wamelazimika kuzuia safari zote za watalii.
Amesema safari hizo zimezuiwa kuanzia jana Machi 20, 2020 ikiwa ni njia ya kupambana na COVID19 na yeyote atakayewasili visiwani humo atakaa karantini kwa siku 14 kwa gharama zake.
Aidha, Waziri Mahmoud amesema sekta ya Utalii katika visiwa hivyo imeathiriwa kwa asilimia 90-95 na italeta athari pia kwa Vijana wanaofanya kazi katika sekta hiyo.
Ameyasema hayo alipokuwa ameenda kumtembelea Mgonjwa wa corona visiwani humo katika Kituo maalumu kilichotengwa kwa ajili ya Wagonjwa wa virusi hivyo kilichopo Kidimni Mkoa wa Kusini Unguja.