Tume ya Sayansi na Teknolojia COSTECH imetoa ruzuku ya Shilingi Bilioni 1.5 kwa mwaka wa fedha 2020/21 kwa ajili ya kufadhili miradi ya ubunifu na utafiti.
Miradi hiyo ni pamoja na miradi 70 ya ya ubunifu chini ya mashindano ya kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na ubunifu MAKISATU, miradi minne ya utafiti, mradi mmoja wa kimkakati Zanzibar na miradi miwili ya kibiashara.
Akizungumza na wabunifu na watafiti katika hitimisho la mafunzo yaliyofanyika kwa siku nne, Mkurugenzi wa COSTECH Dkt. Amosi Nungu amesema washiriki wamefundishwa mambo mbalimbali ikiwemo masuala ya miliki-bunifu, usajili wa haki miliki, mifumo ya biashara na fursa za ujasiriamali.
Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa James Mdoe, amesema serikali kwa mwaka 2020/2025 imedhamiria kukuza Sayansi na Teknolojia kwa kuibua na kuendeleza ubunifu kwa vijana
Aidha, imeelezwa kuwa ili kuhakikisha ruzuku zinatumika kama zilivyodhamiriwa COSTECH itaingia mkataba na mbunifu, pamoja taasisi husika anayotoka mbunifu.