Mshambuliaji Daniel Sturridge wa Liverpool amesema yuko fiti na sasa anataraji kurudi uwanjani mara baada ya kuwa ameanza mazoezi na kikosi cha kwanza na wachezaji wenzie wa Liverpool.

Sturridge ambaye hajakuwa sawa kwa kipindi cha takribani miezi 18 kutokana na kusumbuliwa na majeruhi, amerudi tena upya na anahitaji kutoumia na kufanya kazi ili kujiweka sawa kwa kocha mpya mjerumani Jurgen Klopp.

Akizungumza katika hafla za uzinduzi wa mavazi ya klabu akiwa kama mgeni mualikwa, Sturridge amesifia matunda ya kocha mpya Jurgen Klopp klabuni hapo huku akisema anaona ni wakati mahsusi kwake na kwa klabu.

Liverpool hivi sasa imekuwa ikimtumia mshambuliaji raia wa Ubelgiji Christian Benteke pekee.

Arsene Wenger Amalizana Na Sanchez, Ozil
Mkwasa Awashukuru Watanzania Kwa Kuwapa Somo