Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es Salaam (DCPC) imemtaka mwenyekiti wa chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ,Freeman Mbowe kuomba radhi waandishi wa shirika la Habari TBC.

Taarifa ya DCPC imesema kuwa kitendo alichofanya Mbowe kilikosa busara na ukomavu wa kisiasa pamoja na kiliwadhalilisha na kuwafedhesha waandishi wale pamoja na taaluma ya habari .

“sisi DCPC ni klabu huru ya waandishi wa habari mkoa wa Dar es salaam, wakati tukiendelea kutafakari hatua sahihi za kuchukua kwa kushirikiana na wadau wengine wa habari mkoani humu, inachukua nafasi hii kukemea na kulaani kitendo kile pamoja na kumtaka Mhe. Mbowe kuomba radhi kwa waandishi wale, Televisheni ya taifa, tasnia ya habari, pamoja na Watanzania kwa ujumla,” imesema taarifa hiyo kupitia mwenyekiti wake Irene Mark

TBC ilijikuta matatani katika ufunguzi wa kampeni baada ya Mwenyekiti (CHADEMA), Mbowe, kuamrisha waandishi wa shirika hilo kuondoka viwanja vya Mbagala Zackem jijini Dar es Salama.

Macron awashukia viongozi Lebanon
Suga wa Japan kusaka nafasi ya waziri mkuu Abe