Dereva wa Lori, Nkandi Kanokwa (61), mkazi wa Nzega Mkoani Tabora anashikiliwa na Polisi Mkoani Morogoro kwa tuhuma za kusababisha ajali iliyopelekea kifo cha mtu mmoja na wengine wanane kujeruhiwa.

Chanokwa anadaiwa kuwa chanzo cha ajali hiyo baada ya Lori alilokuwa akilindesha lenye namba za usajili T960 DSV kuhama upande wake wa kushoto kwenda kulia na hivyo kuligonga basi huku Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, ACP Alex Mkama akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

Mkama amesema, katika ajali hiyo, magari matatu, lori lenye namba za usajili T 960 DSV na basi kampuni ya Johanvia lenye namba za usajili T 728 EBT yalihusika.

Aidha, amesema Lori hilo lilikuwa likitoka Musoma kuelekea Dar es Salaam na kwa pamoja yaligongana na gari la Polisi eneo la Kingolwira liliopo Manispaa ya Morogoro katika Barabara Kuu ya Morogoro – Dar es salaam.

Mauaji Wanafunzi 37: 20 wadakwa na Polisi
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Juni 20, 2023