Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ufaransa Didier Deschamps, ameweka wazi kuwa kwa sasa mshambuliaji wa klabu ya Manchester United Mfaransa, Paul Pogba hana furaha ndani ya klabu hiyo.
Mshambuliaji huyo amekuwa si mtu mwenye furaha na kuonekana hapendwi katika uwanja wao wa Old Trafford.
Pogba ambaye yupo na kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa kwa ajili ya michezo ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Colombia na Urusi alionekana kutopendezwa kufuatia kutolewa kwenye mchezo wa kombe la FA wakati timu yake ya Manchester United ikicheza na Brighton jumamosi iliyopita, wakati huo huo hakujumuishwa kwenye kikosi kilicho cheza na Sevilla klabu bingwa ulaya.
Deschamps akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na michezo hiyo ya kirafiki amekiri kuwa Pogba hana furaha na anashindwa kuelewa tatizo na nini kinaendelea kati yake na United.
“Sijazungumza na Paul bado, nauhakika nitasikia mengi kuhisiana na hili. Lakini na uhakika ni kitu ambacho hawezi kukifurahia’’ amesema Deschamps.
Pogba ameanza katika michezo 24 msimu huu chini ya Jose Mourinho ambaye kwa michezo ya hivi karibuni amekuwa akiwachezesha Marouane Fellaini na mchezaji kijana Scott McTominay katika nafasi ambayo amekuwa akicheza Pogba.