Kiungo Mshambuliaji wa Timu ya taifa ya Argentina Angel Di Maria amewaaga rasmi Mashabiki wa taifa hilo baada ya kucheza mchezo wa mwisho kwenye ardhi ya nyumbani mwishoni mwa juma lililopita.

Di Maria ameandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram: “asante, asante na asante mara elfu” kwa mashabiki wa Argentina baada ya kucheza mchezo ambao unatarajiwa kuwa ndio wa mwisho kwake kwenye ardhi ya nyumbani.”

“Nitasema tu asante kwa upendo mkubwa ambao nimepata,” aliandika di Maria kwenye ukurasa wake wa Instagram.
“Siku zote nilikuwa nikiota kila kitu nilichoishi katika usiku huu mzuri. Pengine ilikuwa mechi yangu ya mwisho na jezi ya Argentina nyumbani, na kuweza kusema kuwa ulikuwa usiku mzuri.

“Asante, asante na asante mara elfu.”Sasa niipongeze timu nzima kwa mechi kubwa iliyochezwa, mechi nzuri kwa wote. Tunaendelea kukua na kuwa pamoja. Twende Argentina!!!”Di Maria amecheza mechi 121 na kufunga mabao 24 tangu aicheze kwa mara ya kwanza Argentina dhidi ya Paraguay mwaka 2008.

Mchezaji mwenzake wa Paris Saint-Germain, Lionel Messi ndiye aliyefaidika na pasi ya mabao ya Di Maria, huku Argentina wakiwa tayari wana uhakika wa kwenda Qatar, alipendekeza baada ya mchezo huo afikirie mustakabali wake wa kimataifa baada ya Fainali za Kombe la Dunia.

Di Maria alikuwa na uhakika zaidi katika maoni yake baada ya mchezo huo, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34, akitafakari juu ya “usiku mzuri.”

Kocha Biashara United Mara awasifia washambuliaji wake
Wanawake marufuku kusafiri bila kuandamana na mwanaume