Meneja wa klabu ya Atletico Madrid Diego Pablo Simeone González amesema hakuwahi kusema anaondoka Vicente Calderón Stadium, licha ya baadhi ya vyombo vya habari duniani kuripoti taarifa hizo tofauti kila kukicha.

Simeone alihushwa na taarifa za kuwa tayari kuondoka klabuni hapo baada ya kushindwa kwa mara ya pili katika mchezo wa hatua ya fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya kwa kufungwa na mahasimu wake wa mjini Madrid, Real Madrid mwezi May mwaka huu.

Kwa mara ya kwanza Atletico Madrid walikubali kupoteza mchezo wa fainali wa michuano hiyo dhidi ya Real Madrid mwaka 2014 lakini meneja huyo kutoka nchini Argentina alipambana na kukirejesha tena kikosi chake katika hatua ya fainali msimu uliopita lakini bado ilikua ni bahati mbaya kwake.

Simeone amekanusha taarifa za kutaka kuondoka Vicente Calderón Stadium, baada ya kushindwa kufanya vyema katika mchezo wa hatua ya fainali, alipozungumza na katika moja ya vipindi cha Movistar TV “Espacio Reservado”.

“Wakati yalipotokea matokeo yale, nilikaa na nikafikiria na nilibaini halitokua jambo la busara kuondoka katika kipindi ambacho bado unahitajika Atletico Madrid. Na kama ningefanya hivyo basi nisingekua na amani kwa wakati wote wa maisha yangu,” Alisema Simeone.

“Sikuwahi kusema hadharani ninataka kuondoka. Nilisema nahitaji kufikiria baadhi ya mambo. “Najua mashabiki walishtushwa na taarifa zilizokua zikiandikwa katika vyombo vya habari, lakini nililitambua jambo hilo na nilifahamu nini wanachokohitaji kutoka kwangu,”

“Ni kweli inaumiza, maana kufika katika mchezo wa hatua ya fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya mara mbili mfululizo halafu unapoteza tena kwa mpinzani yule yule inaumiza sana, lakini nilijaribu kujipoza na nikaamini bado nina nafasi ya kufanya vizuri zaidi ya ilivyokua.” Alisema Simeone.

Pep Guardiola Hajaridhishwa Na Usajili Alioufanya
Video: Wanafunzi hewa kusakwa nchi nzima