Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete amemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika hafla ya Mazishi ya Kitaifa ya Rais wa Zamani wa Finland, Hayati Martti Ahtisaari, iliyofanyika Helsinki Novemba 10, 2023.

Akiongea katika wakati wa mazishi hayo, Kikwete alisema Rais Samia anatoa salamu za rambirambi kwa Rais wa Findland, Sauli Niinistö, Familia ya Marehemu na watu wote wa Finland kufuatia kifo cha kiongozi huyo mkubwa duniani.

Aidha, Kikwete aliungana na viongozi mbalimbali walioshiriki mazishi hayo wakimwemo Rais wa Kosovo, Vyosa Osmani na Rais wa Namibia, Hage Geingob na kummwagia sifa Hayati Martti Ahtisaari kwamba alikuwa kiongozi mwenye maono na mpenda amani duniani.

Hayati Martti Ahtisaari aliwahi kuwa Balozi wa Finland nchini Tanzania kuanzia mwaka 1973 hadi 1976 na alikuwa Rais wa Finland kuanzia mwaka 1994 hadi 2000.

Katika vipndi vyote hivyo, Hayati Martti Ahtisaari aliimarisha uhusiano wa Tanzania na Finland katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufanya ziara ya kitaifa nchini Tanzania mwaka 1997 wakati wa Serikali ya Awamu ya Tatu iliyokuwa inaongozwa na Hayati Benjamin Mkapa.

Wahitimu 1,206,995 kujiunga Kidao cha kwanza 2024
Wizara kutoa Chanjo kwa Watoto zaidi ya 2,000