Mbunge wa Vunjo, Dkt. Charles Kimei amesema Serikali ya Chama cha Mapinduzi haina ubaguzi katika suala la utekelezaji wa maendeleo na kuwataka wapinzani kuacha kupinga kila kitu kwani suala hilo linarudisha nyuma nguvu kazi ya Taifa.
Dkt. Kimei ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano maalum na Dar24 Media na kuongeza kuwa, kuwa mpinzani haimaanishi kupinga kila jambo hata kama ni jema na kwa kufanya hivyo wanakuwa hawaikomoi Serikali zaidi ya kuwakosesha wananchi mambo ya msingi ikiwemo maendeleo.
“Vyama vya upinzani vikiwa vinajadili hoja, na sio tu kujadili namna ya kumtoaa kiongozi aliyepo madarakani na kizuri wakipokee Serikali haibagui na ndiyo dhana ya CCM, kuna majimbo mengine yameendelea vizuri licha ya kuwa yanaongozwa na upinzani,” Amesema Dkt Kimei.
Akizungumzia suala la ukimya wake katika vyombo vya Habari, Dkt. Kimei amesema “unapoe elewa mambo halafu ukaona watu wanavuruga unajisemea acha nikae kimya, sitaki kujenga uadui na watu, unaacha watu waseme na kama ni ushauri basi unautoa kwa anayehusika na si kuongea kwenye media nimejifunza kutotoa siri.”