Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango amewataka watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Taasisi zake kuwahudumia wananchi kwa uadilifu ili kujenga uaminifu kwa wananchi na Serikali yao.

Ameyasema hayo wakati alipotembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango katika viwanja vya maonyesho ya Nane nane katika eneo la Ngongo mkoani Lindi.

Amesema kuwa Wizara ya Fedha na Mipango inategemewa na wananchi wengi hivyo ni vyema wahudumiwe vizuri pamoja na kutoa elimu kwa umma vya kutosha ili waweze kuelewa na kuridhika na huduma zinazotolewa na wizara.

“Tujitahidi kuwaelezea wananchi juu ya kazi na huduma zetu ili waweze kuzitumia kwa manufaa yao na Taifa kwa ujumla na tuweze kufikia uchumi wa viwanda kama lengo la Serikali ya Awamu ya Tano ilivyojipangia ” Amesema Dkt. Mpango.

Hata hivyo, Kauli mbiu ya maonyesho hayo ya Nane nane mwaka huu ambayo ni ya 24 kufanyika kitaifa huku yakifanyika mwaka wa nne mfululizo mkoani Lindi inasema “Zalisha kwa tija mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi ili kufikia uchumi wa kati”.

Video: Kenyatta, Odinga mchuano mkali, Waliopiga mabilioni viwanda kitanzani
Kenya: Uhuru aendelea kuongoza, apenya ngome za Odinga