Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amemuagiza Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Singida, Rashid Mandoa kuhakikisha ofisi za halmashauri hiyo zinahamia ndani ya eneo husika kutoka walipo sasa katika manispaa ya Singida.

Ametoa agizo hilo wakati akikabidhi vyeti kwa madiwani wa halmashauri ya Singida waliohitimu mafunzo kuhusu jitihada za jamii kupitia mbinu shirikishi ya fursa na vikwazo kwa maendeleo.

“Ukikaa kwenye nyumba inayovuja ndipo utapata akili na ubunifu wa kutatua changamoto hiyo, ukiangaia wanufaika wa Tasaf wameweza kufanya mambo mazuri kwa pesa kidogo walichonacho, mkurugenzi uige mfano huo, mhamie katika halmasahuri yenu,” amesema Dkt. Nchimbi.

Aidha, amesema kuwa kutohamia katika halmashauri yao kutasababisha halmasahuri hiyo kuvunjwa na hivyo kukosa ajira kwa watumishi huku akiwaeleza madiwani kuwa wataponzwa wa kukosa kura katika uchaguzi ujao.

Hata hivyo, Dkt. Nchimbi amesema kuhusu makao makuu ya halmashauri hiyo baraza la madiwani litachagua makao makuu yao huku akishauri wazingatie eneo ambalo litafaa kwakuwa Halmashauri hiyo inapitiwa na miradi mbali mbali ya kitaifa.

 

 

 

Kanye West atoweka, mashabiki wataka arudi
Mbunge viti maalum awakumbuka wananchi wake