Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro ameruhusu kusafirisha jumla ya kontena 93 ya gundi ( utomvu) ambayo sawa na tani 1,683 iliyokuwa tayari imeshavunwa wakati akitoa tamko la kuzuia usafirishaji wa malighafi hiyo kwenda nchi za nje.

Ametoa kauli hiyo leo Disemba 14, 2021 Jijini Arusha mara baada ya kupokea ushauri kutoka kwa Kamati ya Kumshauri Waziri kuhusu masuala ya misitu kabla ya kufanya mkutano wa Wadau wa mazao ya misitu kuwa gundi hiyo ambayo imekwisha vunwa inapozidi kukaa inapoteza ubora wake na hivyo kutokufaa tena kwa matumizi

” Hii gundi ni ‘Chemicals’ inavyozidi kukaa inabadilika rangi na Wataalamu wamenambia kuwa ikiendelea tu kukaa muda wake unaisha wa matumizi” Amesema Dkt. Ndumbaro.

Gundi ni aina ya utomvu unaogemwa kwenye miti ya kupandwa aina ya misindano ambapo malighafi hiyo husafirishwa kwenda nchi za nje lakini hata hivyo hadi hivi sasa matumizi yake bado hayajaweza kufahamika kuwa inatumikwa kwa ajili ya kutengenezea vitu gani

Hatua hiyo inakuja kufuatia agizo la kusitishwa kuvunwa na kusafirishwa kwa malighafi hiyo kwenda nchi za nje alilolitoa Dkt. Ndumbaro mwezi Oktoba akiwa mkoani Iringa mara baada ya kushindwa kupata maelezo ya kutosha kuhusiana na biashra ya bei ya gundi hiyo pamoja na matumizi yake huko inakosafirishwa nchi za nje hususani China

Katika hatua nyingine, Dkt. Ndumbaro ameendelea kushikilia msimamo wake wa kusitisha zoezi la kuvuna utomvu huo hadi pale Chuo cha Kilimo cha Sokoine ( SUA) pamoja na Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania ( TAFORI) zitakapotoa utafiti wake ambao kwa sasa bado haujakamilika juu ya athari ya miti inayovunwa gundi hiyo

Akifafanua katazo hilo Dkt. Ndumbaro amesema katazo hilo lina manufaa makubwa kwa Watanzania kwa ajili ya kutengeza ajira nyingi kwa wananchi

Serikali yaahidi makubwa sekta ya elimu
Rais Mwinyi afanya uteuzi