Matumizi yasiyo sahihi ya viuatilifu na udaganyifu wa baadhii ya wauzaji wa bidhaa hiyo na mazao ya mimea, yametajwa kuwa kikwazo katika kukabiliana na wadudu waharibifu wa mimea nchini.
Hayo yamebainishwa hii leo Machi 1, 2023 jijini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), Dkt. Joseph Ndunguru wakati akielezea majukumu na utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Mamlaka hiyo.
Amesema uelewa mdogo wa wakulima na wadau wengine juu ya matumizi sahihi ya viuatilifu, na uwepo wa wauuzaji wa Viuatilifu na mazao ya mimea wasio waaminifu imesababisha kuendelea kuwepo kwa wadudu visumbufu wa mimea.
“Matumizi yasiyosahihi ya viuatilifu na udaganyifu wa baadhii ya wauzaji wa viuatilifu changanya na Uelewa mdogo wa wakulima na wadau wengine juu ya matumizi sahihi ya viuatilifu, na uwepo wa wauuzaji wa Viuatilifu na mazao ya mimea wasio waaminifu imesababisha kuendelea kuwepo kwa wadudu visumbufu wa mimea,” amesema Dkt. Ndunguru.
Aidha, Dkt.Ndunguru, ameeleza madhara ya kutumia viuatilifu visivyo sahihi kwa wakulima kuwa inawaongezea gharama kwa sababu mkulima analazimika kutumia viuatilifu vingi na inaathiri afya yake na mazingira kwa ujumla.
“Madhara ni mengi ndio maana tulitilia mkazo kwa kuwajengea uelewe wakulima juu ya matumizi sahihi ya viuatilifu sababu wanapopulizia viuatilifu visivyosahihi vinawajengea usugu wadudu waharibifu na kuuwa wadudu rafiki wa mimea,” amesema Dkt.Ndunguru.