Jeshi la Polisi Nchini, limempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha utaratibu wa mafunzo ya Jeshi hilo kwa kuwawezesha vitendea kazi ikiwa nipamoja na kuondoa makato ya fedha ya chakula kwa askari walioko mafunzoni, katika vyuo mbalimbali vya Jeshi hilo.

Hayo yamesemwa hii leo Machi 1 2023 na Kamishina wa opereshi na mafunzo ya Jeshi la Polisi Nchini, Awadh Juma Haji wakati akiongea na Wanafunzi wa Kozi ya Uofisa na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, katika chuo cha Taaluma ya Polisi, Dar es salaam.

Amesema Askari hao wanatakiwa kujitoa kikamilifu katika mafunzo hayo kwa kupokea mafunzo yanayotolewa na walimu ndani ya darasa na katika medani za kivita ili kutimiza adhima ya amiri Jeshi ya kujenga mazingira rafiki katika kozi za Jeshi hilo.

Sambamba na hilo ujio wake pia ni katika kuungana na kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi Jamal Rwambow ambae ni mstaafu wa Jeshi la Polisi ambapo amebainisha kuwa kamishina uyo amejikita katika uandishi wa vitabu lengo likiwa ni kuikomboa jamii kupitia uandishi wake na kushauri Jeshi la Polisi katika utoaji huduma kwa wananchi.

Pia katika hafla hiyo amepata wasaa wa kuzindua kitabu kilichoandikwa Salam za marehemu nakuwaomba askari kusoma vitabu hivyo ambavyo vina toa dira na mweleko sahihi katika kutoa huduma kwa jamii.

Kwa upande wake kamishina msadizi mwandamizi mstaafu Jamal Rwambow amesema kuna baadhi ya watu wanasimamia kazi za upelelezi ambapo amebainisha kuwa kuna watu hao hawana uwezo mkubwa wa maswala ya upelelezi na kusema kuwa Jeshi hilo linaouwezo mkubwa wa upelelezi hivyo ameiomba serikali kuliwezesha kifedha hasa kitengo cha upelelezi ili kuwa naufanisi mkubwa.

Nae mkuu wa chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam Kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi Daktari LAZARO MAMBOSASA amesema kuwa anamshukuru mkuu wa Jeshi la Polisi kwa namna anavyopigania maslahi ya askari na kuahidi kuwa wao kama wakufunzi watahakikisha wanasimamia mafunzo hao kwa weledi mkubwa.

Dkt. Ndunguru: Udanganyifu chanzo wadudu waharibifu wa mimea
Usalama kazini: GGML yashinda tuzo Kimataifa