Misingi imara ya udhibiti wa hali ya usalama katika utendaji kazi ndani na nje ya Mgodi wa Geita Gold Mining Limited – GGML, imeendelea kuifanya kampuni hiyo kuandika historia duniani baada ya kushinda  kwa mara ya nne mfululizo tuzo ya kimataifa ya usalama mahala pa kazi.

Akizungumzia ushindi huo katika mahojiano maalumu mkoani Geita, Meneja Mwandamizi wa Afya, Usalama, Mazingira na Mafunzo wa GGML, Dkt. Kiva Mvungi alisema kwa tuzo hiyo ni wazi AGA imeitambua GGML kama kampuni kinara inayofanya vizuri katika masuala ya usalama Duniani.

Meneja Mwandamizi wa Afya, Usalama, Mazingira na Mafunzo wa GGML, Dkt Kiva Mvungi (wa pili kulia) pamoja na watendaji wa idara ya afya na usalama kutoka Geita Gold Mining Limited wakifurahia ushindi wa nne mfululizo katika tuzo ya kimataifa ya usalama mahala pa kazi. Kampuni hiyo imeiongoza Tanzania imezipiku nchi za Australia, Ghana na Afrika Kusini.

AGA ambayo imeorodheshwa katika masoko ya hisa ya Johannesburg, New York, Australia na Ghana inamiliki migodi katika nchi za Australia, Columbia, Argentina, Brazil, Ghana na Tanzania. Katika nchi zote hizo,GGML au Watanzania kwa ujumla ndio vinara wa kuzingatia masuala ya usalama mahala pa kazi.

Alisema tangu wameanza kutumia mfumo huo wa kuwasikiliza zaidi wafanyakazi, mafanikio yamekuwa makubwa katika utendaji kazi. Anatolea mfano kuwa zaidi ya miaka 10 hawajapoteza maisha ya mfanyakazi yeyote kazini, lakini zaidi ya miaka mitano hakuna mfanyakazi aliyeumia kiasi cha kushindwa kuingia kazini. Pia wamekaa zaidi ya miaka minne bila ya kuwa na mtu aliyeumia kazini.

Meneja Mwandamizi wa Afya, Usalama, Mazingira na Mafunzo wa GGML, Dkt Kiva Mvungi.

Akizungumza ushindi huo wa tuzo nne mfululizo, Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Terry Strong aliipongeza timu nzima ya idara ya afya, usalama na mazingira pamoja na wafanyakazi wote wa GGML kwa kudumisha usalama wao ndani na nje ya kampuni ambapo mbali na tuzo hiyo ya kimataifa ya usalama, GGML pia ilipata tuzo ya utendaji bora wa jumla.

Mmoja wa wafanyakazi wa idara hiyo ya usalama, afya na mazingira ndani ya GGML, Dkt. Subira Joseph ambaye amefanya kazi ndani ya kampuni hiyo kwa zaidi ya miaka 10 kama daktari kwenye kituo cha afya cha GGML pamoja na Josephine Kimambo ambaye ni mhandisi wa mazingira, walisema ushindi mfululizo wa tuzo hiyo, umewafanya waone wanafanya kazi kwenye mazingira salama.

Serikali yaboresha mazingira utoaji taaluma Jeshi la Polisi
Serikali yakabidhi eneo ujenzi Kituo kudhibiti maafa