Serikali, imekabidhi eneo la ujenzi wa majengo ya kituo cha Taifa cha kudhibiti Maafa kwa Mkandarasi, Kiure Engineering Limet, lilipo Nzunguni Jijini Dodoma ukihusisha ujenzi wa majengo ya maghala kwa awamu ya kwanza inayoendelea kwa sasa.

Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, wakati wa Hafla ya  makabidhiano ya kituo hicho,  Mkurugenzi wa Utawala na Rasimali watu kutoka  Ofisi hiyo, Stella Mwaiswaga amesema mradi huo wa ujenzi wa kituo hicho, ambapo katika awamu ya pili utahusisha majengo ya maghala na majengo mengine ya uendeshaji yatajengwa kulingana na upatikanaji wa fedha.

Mkurugenzi wa Utawala na Rasimali watu, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Stella Mwaiswaga katika eneo la ujenzi.

Amesema, Ujenzi huu wa awamu ya pili unaotarajiwa kukamilika kwa kipindi cha miezi kumi na mbili, utagharimu kiasi cha zaidi ya shilingi 8,850,000,000 ikiwa ni gharama za mkandarasi zinazojumuisha kodi ya ongezeko la thamani, VAT.

Awali akiongea katika makabidhiano hayo, Mhandisi wa mradi kutoka Ofisi ya waziri Mkuu sera Bunge na Uratibu, Joseph  Muhamba alisema lengo la serikali ni kuwa na  kituo hicho ili kuwawezesha watendaji wake kufanya kazi katika mzingira wezeshi.

Usalama kazini: GGML yashinda tuzo Kimataifa
Uchaguzi Nigeria: Tinubu Rais mteule, wapinzani wamkataa