Kocha mkuu wa timu ya taifa ya DR Congo, Florent Ibenga amatangaza kikosi imara kwa ajili ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars machi 27,2018.
Ibenga amewaita wachezaji wengi wanaocheza barani Ulaya akiwemo mchezaji ghali zaidi barani afrika kwa hivi sasa, Cedric Bakambu aliye jiunga na miamba ya China Beijing Guoan kwa Euro million 65 akitokea klabu ya Villarreal.
Aidha, katika kikosi hicho Ibenga amewajumuisha Bolasie Yannick, Chancel Mbemba na Masuaku Arther ambao wote wanachezea ligi kuu nchini Uingereza.
Taifa stars itawakaribisha DR Congo kwenye mchezo huo wa kirafiki ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kucheza michezo ya kufunzu michuano ya mataifa ya Afrika mwaka 2019, ambapo Tanzania ipo kundi L pamoja na Lithoto, Uganda na Cape Verde.
Wachezaji wengine walioitwa ni pamoja na magolikipa, Parfait Mandanda (Charleroi,France), Joel Kiassumbua (Lugano,Italy) na Matampi Ley.
Walinzi akiwa Issama Mpeko (TP Mazembe), Ikoko Jordan (EAG, France), Nsakala Fabrice (Alayanspor,Turkey), Ngonda Glody (AS Vita Club), Masuaka Arthur (West Ham, England). Chancel Mbemba (Newcastle United, England), Moke Will (Konyaspor, Turkey), Bangala Yannick ( AS Vita), Luyindama Christian (Standard,Belgium), Mulumbu Youssouf (Kilmanock, Scotland), Lema Mabidi (Raja, Morrocco).
Viungo akiwa Kebano Neeskens (Fulham, England ), Giannelli Imbula (Toulouse, France), Maghoma Jacques (Birmingham, England ), Kakuta Gael (Amiens, France).
Washambuliaji ni Balasie Yannick (Everton, England), Kabananga Junior (Al Nassr, Saudi Arabia), Mubele Fiemin (Touloise, France ), Paul Jose Mpaku (Standard Liege, Belgium), Cedric Bakambu (Beijing, China), Afobe Benik (Wolves,England ) Assombalonga Britt (Middlesbrough, England),