Mshambuliaji wa Azam FC Prince Dube ana matarajio hafifu ya kuwakabili Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, kwenye mchezo wa Ligi Kuu utakaochezwa keshokutwa Jumatano (Julai 14), Uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Dube anapewa nafasi ndogo ya kuonekana kwenye mchezo huo, kufuatia majeraha yanayomkabili kwa kipindi kirefu, na sasa benchi la ufundi linasubiri ripoti ya mwisho la jopo la madaktari wa klabu hiyo, ili kufahamu kama atatumika dhidi ya Simba SC.

Mshambuliaji huyo kutoka nchini Zimbabwe alikosa mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya Nusu Fainali dhidi ya Simba SC mjini Songea mkoani Ruvuma, ambapo alikuwa jukwaani akitazama mchezo huo uliomalizika kwa Azam FC kufungwa bao 1-0.

Dube kwenye mabao 48 amehusika katika mabao 19, akiwa amefunga mabao 14 na kutoa pasi tano za mabao, ana umhimu mkubwa wa kuwa sehemu ya kikosi cha Azam FC kitakachoivaa Simba SC kutokana na hitaji la timu yake la kusaka ushindi, ili kuweza kutimiza lengo la kumaliza nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu.

Ikiwa imecheza michezo 32 ya Ligi Kuu msimu huu 2020/21 na kukukusanya alama 64, Azam FC inapaswa kushinda michezo yake miwili iliyosalia kwa mabao mengi zaidi huku ikisubiri matokeo ya Young Africans.

Young Africans ipo nafasi ya pili na ina michezo miwili mkononi ikiwa na alama 70, kwa upande wa mabao klabu hiyo kongwe katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati imefunga mabao 50 huku Azam FC ikiwa imefunga mabao 48.

Young Africans yatamba kuzifunga Ihefu, Dodoma Jiji
Gomes atuma salamu kwa waliobaki