Uongozi wa Geita Gold uko kwenye mazungumzo na beki wa pembeni David Kameta ‘Duchu’ kwa ajili ya kumsajili moja kwa moja, baada ya kumaliza mkataba wa mkopo mwishoni mwa msimu huu.

Duchu alisajiliwa Geita Gold FC mwanzoni mwa msimu huu, akitokea Simba SC, ambako alikosa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha Mabingwa hao wa zamani wa Tanzania Bara.

Taarifa zinaeleza kuwa, mazungumzo baina ya Beki huyo na Uongozi wa Geita Gold yamefikia pazuri, na wakati wowote kuanzia sasa, atakamilisha taratibu zote za kusajiliwa jumla.

Duchu alijiunga na Simba SC akitokea Lipuli FC ya mkoani Iringa msimu wa 2020/21, lakini hakubahatika kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza, kufuatia uwepo wa Beki Shomari Kapombe ambaye amekuwa na uhakika wa kucheza mara kwa mara.

DC atumia trekta kuwafikia wananchi
Okrah amaliza vibaya Ghana, kutua Dar es salaam