Bondia Abdallah Pazi ‘Dulla Mbabe’, ameibua kizaazaa baada ya kutaka kumshushia kipigo dereva wa basi la daladala jijini Dar es salaam.

Tukio hilo lilitokea, katika eneo la Banana jana Ijumaa (Mei 12), majira ya saa 2:30 asubuhi.

Chanzo ni dereva wa Daladala hilo linalofanya safari zake kati ya Kigogo Sokoni-Machinga Complex kulichomekea gari la Dulla na kuanza kumtolea lugha chafu bondia huyo.

Kufuatia hiyo, ilimlazimu kusimamisha hali Dulla gari na kumfuata dereva huyo kisha kutaka kumchomoa katika gari na kusababisha kizaa zaa.

Abiria waliokuwemo katika Daladala lenye namba za usajili T350 CVQ walianza kumtetea dereva asipate kichapo, wakati huo Dulla akiwa kwa ghadhabu amefura akilalamika kutukanwa na kuchomekewa.

Hata hivyo Dulla baada ya jitihada za kumchomoa dereva huyo ambaye aling’ang’ania mlango kushindikana alirejea katika gari lake na kuondoka.

Dulla amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa licha ya kuondoka eneo la tukio lakini atachukua hatua zaidi kwa sababu alidhalilishwa kwa kutukanwa matusi.

“Nitaripoti polisi. Nimechukua namba za gari hilo. Alinitolea lugha chafu bila makosa. Tena lugha mbaya mno bila kujali ndani ya basi lake kuna watoto,” amesema Dulla

Ongezeko la wahamiaji laishtua White House
Mengi usiyoyajua kuhusu historia ya Benard Membe