Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Ubelgiji Eden Hazard awaomba radhi Mashabiki wa Real Madrid, ambao hawajafurahishwa na kiwango chake tangu alipowasili klabuni hapo.
Hazard alisajiliwa Real Madrid mwaka 2019 akitokea Chelsea ya England kwa ada ya uhamisho Euro Milioni 100, huku akiitumikia klabu hiyo ya Santiago Bernabeu katika michezo 51 na kufunga mabo manne.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 31, amesema anajua tangu aiposajiliwa klabuni hapo, hajaonyesha kiwango kilichotarajiwa na wengi hivyo hana budi kuomba radhi.
Amesema kadri atakavyozidi kuwepo Real Madrid atajitahidi kupambana na kurejea katika kiwango chake ili kuisaidia Klabu kufikia malengo yake kuanzia msimu huu 2022/23.
Hata hivyo Hazard amekuwa na wakati mgumu wa kucheza mara kwa mara kwenye kikosi cha Real Madrid, kutokana na majeraha yanayomuandama, hali ambayo imekua ikimuwe nje kwa muda mrefu.
“Mashabiki wa Madrid, samahani. Sio rahisi, lakini nataka kucheza zaidi.”
“Nikiwa Chelsea, nilicheza michezo 100, bila majeraha. Nikiwa Madrid, nina majeraha” amesema Hazard.
Eden Hazard anatarajiwa kukiongoza kikosi cha Ubelgiji kwenye Fainali za Kombe la Dunia zitakazoanza kurindima nchini QATAR Jumapili (Novemba 20).