Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Uholanzi ‘Oranje’ Aloysius Paulus Maria “Louis” van Gaal, amehoji tena uamuzi wa kuifanya Qatar kuwa mwenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia, huku akisifu maandalizi mazuri ya vifaa na miundombinu katika nchi hiyo ya Kiarabu.

Van Gaal mwenye umri wa miaka 71, aliwahi kusema kuwa uamuzi ule “unachekesha” na hivi sasa ameongeza na kudai kuwa Qatar ni nchi ndogo sana kuwa wenyeji wa mashindano hayo makubwa na pia nchi hiyo haina urithi wa soka.

“Nia ya FIFA ilikuwa ni kuzihamasisha na kuziendeleza nchi zingine, ndio maana tumekuja kucheza hapa, lakini nchi za soka zina uzoefu zaidi na kila kitu, inawezekana pia kuzihamasisha nchi zingine kwa njia nyingine zinazofaa, sio kwa uamuzi kama huu.” amesema Van Gaal

Tayari kikosi cha Uholanzi kimeshawasili QATAR kwa Fainali za Kombe la Dunia zitakaanza kurindima Jumapili (Novemba 20).

Uholanzi imepangwa Kundi A na wenyeji QATAR, Ecuador na Senegal.

Kikosi cha Uholanzi kinaundwa na Walinda Lango Justin Bijlow (Feyenoord), Andries Noppert (Heerenveen) na Remko Pasveer (Ajax Amsterdam)

Walinzi: Nathan Ake (Manchester City), Daley Blind (Ajax), Virgil van Dijk (Liverpool), Denzel Dumfries (Internazionale), Jeremie Frimpong (Bayer Leverkusen), Matthijs de Ligt (Bayern Munich), Tyrell Malacia (Manchester United), Jurrien Timber (Ajax) na Stefan de Vrij (Inter Milan)

Viungo: Steven Berghuis (Ajax), Frenkie de Jong (Barcelona), Davy Klaassen (Ajax), Teun Koopmeiners (Atalanta Bergamo), Marten de Roon (Atalanta Bergamo), Xavi Simons (PSV Eindhoven) na Kenneth Taylor (Ajax)

Washambuliaji: Steven Bergwijn (Ajax), Memphis Depay (Barcelona), Cody Gakpo (PSV), Vincent Janssen (Antwerp), Luuk de Jong (PSV), Noah Lang (Club Brugge) na Wout Weghorst (Besiktas)

Museveni: 'Lockdown' imesaidia kupunguza Ebola
Eden Hazard aomba RADHI Real Madrid