Shirikisho la soka Barani Afrika limeahirisha zoezi la Droo ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Barani Afrika Hatua ya Makundi.

Droo ya Hatua ya Makundi ya Michuano hiyo ilipangwa kufanyika leo Jumatano (Novemba 16) mjini Cairo nchini Misri, lakini Shirikisho la Soka Barani Afrika CAF, kupitia Tovuti yake limetoa taarifa za kuahirisha zoezi hilo.

Hata hivyo CAF haijatoa sababu zozote za kuahirishwa kwa zoezi hilo, ambalo lilikua linasubiriwa kwa hamu kubwa na wadau wa soka Barani Afrika hususan wale wa nchi zilizoingia klabu kwenye hatu ya Makundi.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa tarehe mpya ya kupangwa kwa Droo ya Hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Barani Afrika itatangazwa baadae.

Taarifa iliyochapishwa na CAF kupitia Tovuti yake imeeleza: Droo ya Hatau ya Makundi Klabu Bingwa na Kombe la Sirikisho imeahirishwa.

Awali droo hiyo ilipangwa kufanyika Jumatano, 16 Novemba 2022.

Tarehe mpya na muda vitatangazwa baadae.

CAF inaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza kutokana na mabadiliko haya.

Imetolewa na Idara ya mawasilino:

Mawasiliano ya CAF

PPRA yawapa ujumbe Maafisa Maendeleo, Wananchi kuneemeka
PICHA: TFF, UNFPA zaingia makubaliano DAR