Malinda mlango mashuhuri wa kikosi cha Misri Essam El Hadary, ataweke rekodi mpya kwenye michuano ya mataifa ya Afrika (AFCON 2017).
mlinda mlango huyo ambaye anaitumikia klabu ya Wadi Degla, amejumuishwa kwenye kikosi cha mwisho cha wachezaji 23 cha Misri ambacho siku si nyingi kitakuwa nchini Gabon kwenye michuano ya AFCON.
Kutokana na kujumuishwa huko, El Hadary ambaye baadae mwezi huu atafikisha miaka 43 ya kuzaliwa kwake, anakwenda kuweka rekodi ya kuwa mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kuwahi kuwemo kwenye michuano ya AFCON.
Anavunja rekodi iliyoweka mwaka 2006 na raia mwezake wa Misri, Hossam Hassan aliyeshiriki michuano ya AFCON akiwa na umri wa miaka 39.