Klabu ya Arsenal inajiandaa kutangaza kukamilisha taratibu zote za kumsajili beki wa kushoto wa Hednesford Town, Cohen Bramall.
Bramall mwenye umri wa miaka 20 amejikuta akiingia kwenye mikono ya meneja Arsene Wenger, baada ya kuonyesha kiwango bora cha usakataji kabumbu katika kipindi chote cha majaribio yake yaliyoanza kabla ya siku kuu ya mapumziko ya mwishoni mwa mwaka.
Habari zaidi zinasema Bramall ambaye kiuchezaji anafananishwa na Ashley Cole tayari ameshafuzu vipimo vya afya na anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka miwili na nusu wa kuichezea Arsenal huku klabu yake ya Hednesford Town inayoshiriki ligi daraja la saba nchini England ya Evo-Stik Northern Premier League, ikitarajiwa kupokea ada ya uhamisho ya £40,000.
Cohen Bramall mwenye jezi nyeupe.
Kabla ya kutua Arsenal kwa majaribio, Bramall pia aliwahi kufanya majaribio katika vilabu vya Crystal Palace na Sheffield Wednesday.