Klabu ya Leicester City inatarajiwa kumsajili kiungo wa kati wa klabu ya KRC Genk ya Ublegiji Wilfred Ndidi kwa Pauni Millioni 15.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa, Klabu hizo tayari zimekubaliana kuhusu uhamisho wa mchezaji huyo na kilichosalia ni upatikanaji wa kibali chake cha kufanyia kazi katika ligi hiyo ya England.

Chipukizi huyo mwenye umri wa miaka 20 kutoka Nigeria, atatia saini mkataba wa miaka mitano na nusu endapo atakapokamilisha uhamisho wake.

Leicester,tayari wamethibitisha kwenye tovuti yao kuwa klabu hizo zimeafikiana na tayari Ndidi amefanyiwa uchunguzi wa kimatibabu tayari.

“Ndidi anatarajiwa kukamilisha utaratibu wa kuhamia Leicester City baadae juma hili.”

Ndidi aliwasaidia Genk kumaliza kileleni mwa kundi lao la Europa League msimu huu na kufuzu kwa hatua ya mtoano.

El Hadary Kuweka Rekodi Ya Kipekee AFCON 2017
Bocco: Young Africans Ina Kikosi Bora