Mkuu wa mkoa wa Iringa, Halima Dendego amesema upatikanaji wa nishati safi kwa watanzania inawezekana kutokana na uwepo wa vyanzo vingi vya uzalishaji pamoja na kuongeza utoaji wa elimu kwa jamii nzima huku akiahidi kuweka kipaumbele katika kuhamasisha wananchi mkoani humo kupata nishati safi ya kupikia.
Dendego ameyasema hayo, wakati wa mjadala wa Kitaifa wa Nishati safi ya kupikia uliofanyika kwa siku ya jijini Dar es salaam na kusisitiza umuhimu umuhimu wa elimu juu ya masuala ya nishati kwa Taifa ili kuweza kufanikisha lengo lililokusudiwa.
Aidha katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa amesema uharibifu wa misitu hauchangiwi na ukataji wa kuni na mkaa pekee, bali hata shughuli za Kilimo ambazo hazina mpangilio maalumu zinazohusisha uharibifu wa misitu.
Mjadala huo wa Kitaifa wa Nishati safi ya kupikia ulioanza Novemba 1 na kuhitimishwa Novemba 2, 2022, ulifunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.