Serikali ya nchi ya Urusi, imesema imedhamiria kuzuia uwezekano wa kutokea kwa vita vya nyuklia Duniani, na kwamba imeweka jitihada za kuepusha makabiliano ya nyukllia, baina ya madola yanayomiliki silaha hizo hatari ulimwenguni.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Wizara ya mambo ya kigeni ya Urusi, mjini Moscow, imesema bado imejizatiti katika kuheshimu ahadi ya kuepusha kutokea vita vya nyuklia iliyotolewa na viongozi wa mataifa matano yenye silaha za nyuklia Januari 2022.

Urusi, imesema imedhamiria kuzuia uwezekano wa kutokea kwa vita vya nyuklia duniani. Picha: Sky News.

Aidha, Urusi pia imetangaza kuwa inarejea kwenye mkataba wa kusafirisha nafaka ya Ukraine baada ya kujitoa mwishoni mwa wiki iliyopitia katika uamuzi uliotishia kuongeza mzozo wa upatikanaji chakula duniani.

Hata hivyo, Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema inarejea kwenye mkataba huo baada ya kupokea hakikisho la maandishi kutoka Ukraine, kwamba nchi hiyo haitotumia njia za kusafirisha nafaka kwenye Bahari Nyeusi kwa shughuli za kijeshi.

Elimu kusaidia uzalishaji wa Nishati: Dendego
Serikali kuweka sera wezeshi sekta ya Nishati