Mjumbe maalumu wa Umoja wa Afrika (AU), na Rais wa zamani wa Nigeria, Olusegun Obasanjo amesema pande zinazohasimiana nchini Ethiopia zimekubaliana rasmi kusitisha moja kwa moja uhasama huku kukiwa na wasiwasi endapo Serikali ya Eritrea itayaheshimu makubaliano hayo.

Obasanjo ametoa tangazo hilo, wakati akiarifu kwa mara ya kwanza matokeo ya mazungumzo ya amani nchini Afrika Kusini na kuongeza kuwa serikali ya Ethiopia na mamlaka za jimbo la Tigray wameagiza upokonyaji wa kupangwa wa silaha na usio na vurugu.

Ujumbe maalumu wa Umoja wa Afrika uklioongozwa na Rais wa zamani wa Nigeria, Olusegun Obasanjo (wa tatu kulia), ukiwa na wawakilishi wakuu wa pande zinazohasimiana kwenye mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Ethiopia na Tigray. Picha: Phill Mgakoe/ AFP.

Makubaliano mengine ni pamoja na kurejeshwa kwa sheria na utulivu na huduma, na kuruhusu ufukishwaji wa huduma za kibinaadamu huku akisema “Huu sio mwisho wa mchakato wa amani ndio kwanza tunauanza. Utekelezaji wa mkataba wa amani uliotiwa saini hii leo ni muhimu kwa mafanikio ya mchakato huu.”

Kiongozi wa ujumbe wa serikali ya Ethiopia kwenye mazungumzo hayo, Redwan Hussein amesema ni wakati kwa pande zote kuheshimu makubaliano, kauli inayoungana na kiongozi wa upande wa Tigray, Getachew Reda lakini akisisitiza kwamba makubaliano yaliyofikiwa yasichukuliwe kirahisi.

Serikali kuweka sera wezeshi sekta ya Nishati
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Novemba 3, 2022