Umoja wa Mataifa (UN), umesema vyombo huru vya habari ni chachu muhimu ya kuhakikisha utekelezaji wa demokrasia, kufichua maovu na kukabili matukio mengi ya Dunia hii yenye changamoto na kusongesha ajenda ya maendeleo endelevu SDG’s.

Rai hiyo, imetolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres ambaye ameongeza kuwa, “Bado waandishi wa habari zaidi ya 70 wameuawa mwaka huu sababu ya kutimiza wajibu wao katika jamii.”

Guterres ameongeza kuwa, “Na uhalifu huu kwa kiasi kikubwa haujapatiwa suluhu , wakati huohuo waandishi wengi wa habari wanashikiliwa vizuizini , vitisho vya kuwafunga vinaendelea, ukatili dhidi yao unaendelea na idadi ya wanaouawa inaongezeka.”

Picha ya Rais Samia Suluhu Hassan, iliyopigwa siku ya Uhuru wa vyombo vya Habari Diniani.

Aidha, amesisitiza kwamba, “Ongezeko la habari potofu, uonevu mtandaoni na matamshi ya chuki, hasa dhidi ya waandishi wa habari wanawake, vinachangia kuwakandamiza wafanyakazi wa vyombo vya habari kote duniani kote.”

Kwa upande wake, Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO, kupitia takwimu zake mpya zilizotolewa Novemba 2, 2022 zinaonyesha kwamba duniani kote ukwepaji sheria kwa uhalifu wa mauaji dhidi ya waandishi wa habari uko katika kiwango cha juu kwa asilimia 86.

Ripoti hiyo, pia inaonyesha hakuna mahala salama kwa waandishi wa habari na imeendelea kubainisha kuwa mwaka 2020-2021 miongoni mwa waandishi wa habari 117 waliouawa kwa sababu ya kazi yao, 91 kati yao au asilimia 78% wakiuawa wakiwa nje ya saa za kazi.

Vita Ukraine: Korea Kaskazini yadaiwa kuisaidia Urusi
Elimu kusaidia uzalishaji wa Nishati: Dendego