Taarifa za kijasusi za Marekani, zimesema Korea ya Kaskazini inaisaidia Urusi katika vita dhidi ya Ukraine kwa kuipatia makombora na mizinga ili kufanikisha ushindi katika vita hiyo iliyoanza mapema mwaka huu.

Kwa mujibu wa Data, zilitolewa miezi miwili baada ya mashirika ya kijasusi ya Marekani kueleza tuhuma za Urusi, zinasema Moscow inaweza kununua mamilioni ya makombora kutoka Korea Kaskazini ili kurahisisha mashambulizi yake.

Hata hivyo, taarifa hizi zinakuja wakati ambapo mwezi Septemba 2022, Korea Kaskazini ilikanusha madai ya kutoa makombora kwa Urusi, na bado hakuna ushahidi wowote wa madai hayo.

Puttin akiwa na Kim Jong Un. Picha na Diplomat.

Hata hivyo, mtazamo wa Wamarekani wa vifaa vya kijeshi kutoka DPRK, pamoja na ununuzi wa ndege zisizo na rubani na silaha zingine kutoka Iran, zinaonyesha kuwa baada ya miezi minane ya vita, hifadhi ya silaha za kawaida za Urusi zilianza kuisha.

Hivi karibuni, Mkurugenzi wa Ujasusi wa Kitaifa wa Marekani, Euryl Haynes alisema, “Udhibiti wa usafirishaji unalazimisha Urusi kugeukia nchi kama Iran na Korea Kaskazini kwa usambazaji wa ndege zisizo na rubani, makombora ya mizinga na makombora mengine.”

Amesema, uungaji mkono wa Iran na Korea Kaskazini kwa Urusi hautabadili mkondo wa vita ingawa usambazaji wa silaha bado unaweza kusaidia Urusi kuendelea na vita vya muda mrefu.

Mapya yaibuka maambukizi Homa ya Nyani
Uhuru wa vyombo vya Habari wachangia Demokrasia