Msichana Miheret Tadesse kutoka Ethiopia, amefanikiwa katika kampeni yake anayoiendesha ya jukwaa la wasichana wasiotaka kukeketwa shuleni kupitia klabu yao iitwayo ‘Uncut Girls’.
Wasichana hao wameunda Klabu hiyo ili kuelimisha wenzao, kuhamasisha familia kubadilisha mtazamo wao wa mila hiyo potofu ya ukeketaji au FGM, na kutetea haki za wasichana katika jamii.
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, leo Machi 8, ni siku ya wanawake duniani yenye kauli mbiu “Wakati ni Huu: Wanaharakati wa Mijini na Vijijini wabadili maisha ya Wanawake.
Kampeni ya wasichana hao imekuwa na mafanikio na kupitia siku ya leo, wamekuwa wakitoa elimu na kueleza adhari za kukeketwa pamoja na manufaa ya kutokeketwa kwa binti.